BALAA LA PHIL JONES “ANAOGOPA SANA LIFTI” - SPORTSTAIN

SPORTSTAIN

Stay with us. Be informed

Monday, 18 September 2017

BALAA LA PHIL JONES “ANAOGOPA SANA LIFTI”

Mlinzi kisiki wa Manchester United, Phil Jones

Ni kweli na wala usije kushangaa hata wazaliwa wa ng’ambo pia wanaogopa vyombo vya kiteknolojia.
Eti yule beki wa kati wa Man United, Phil Jones anaogopa sana kupanda lifti “elevator,” anaona ni bora atumie chombo hicho awapo nyumbani England tu lakini kamwe hathubutu nje ya nchi yake na siku zote hutumia ngazi.
“Nikienda ng’ambo, situmii kabisa lifti, lakini nikiwa England huwa sina hofu, na sithubutu niwapo nje ya nchi”
“Nilipokuwa mdogo niliwahi kwenda sikukuu nchini Greece na tulikwama kwenye lifti kwa saa kadhaa”

“Ilitisha sana, nilijihisi kama nimefungiwa sehemu ya kutisha”

Phil Jones katika sura ya kushtukizwa baada ya Sergio Aguero kuweka mpira kambani kwenye mpambano baina ya Man U dhidi ya Man City

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad