Na: Davis Mwakalosi
Dunia imejaliwa zawadi
ya vitu na watu wenye thamani kubwa
sana, kiasi kwamba wapo wataalam wa film industry wanaendelea kutafuta kila namna mpya na bora ya kutengeneza movies kubwa na hata ndogondogo ili kuburudisha, kusisimua halikadharika kuelimisha.
Kuna vitu matata bado
vinaendelea kutengengezwa na kupakuliwa kila uchao mbali ya kuwa tumebakiza miezi michache kuhitimisha mwaka (insha'Allah), Sportstain itaendelea kukufahamisha mengi.
Kwasasa,
hebu ziangalie hizi ambazo bila shaka utazipenda kama bado hujaziona.
1.
The Hitman Bodyguard.
![]() |
| Samuel L. Jackson |
Samuel L. Jackson huyu
ni actor ambaye daima haifanyii makosa kazi yake. Karibu movie zake zote
ni babkubwa. Movie hii kwa surprise kubwa mara baada ya kuachiwa tu tayari copy
yake ya HD imetapakaa sokoni kwa kasi ya moto wa petrol mwituni. Inamhusu story
ya bodyguard mmoja mkubwa sana duniani amepata mteja mpya ambaye ni hitman “muuaji
wa kukodi” anayekabiliwa na kesi kwenye Mahakama ya Kimataifa. Lakini mlinzi na
mlindwaji wameshawahi kutofautiana siku za nyuma na wanatakiwa wayazike yaliyopita na wasonge mbele pamoja.
2.
The Bad Batch.
Filamu hii ni ya Jason Momoa,
aliyechecheza kama Khal Drogo kwenye Game
of Thrones na Keanu Reeves wa The Gun
Fu. Hadithi ya movie hii inauwezo mkubwa sana wa kuteka akili yako mtazamaji.
Inamhusu binti mmoja ambaye anageuka kuwa windo la wala nyama, anapoteza mkono na mguu katika
tukio la kuwindwa. Ili kujilinda asishindwe na hatimaye kuliwa nyama, anaamua
kupambana kijeshi na kumpata mpenzi ambaye anatokea kwenye familia ya wala
nyama za watu (Jason Momoa).
3. Baywatch.
Kwasasa ni kama vile
The Rock yupo kwenye kila movie. Na kazi yake mpya iliyopo sokoni kwasasa Baywatch inamambo mengi na inafurahisha
sana. Inafaa sana hasa wakati unapokuwa bored na unahitaji kutazama kitu
ambacho kitakachokuletea uchangamfu. Inamhusu mlinzi mmoja matata sana Mitch Buchannon,
wanagundua genge la wauza dawa za kulevya ambao ni hatari kwa mustakabali wa
kisiwani wanapoishi.
4.
Free Fire.
Ni movie iliyosheheni
ujasiri, na vituko vya kuvunja mbavu. Nisimalize kila kitu, tafadhari isake na
hakikisha unakopo lako la popcorn wakati unaitazama.
5.
Baby Driver.
Bila shaka tunakubaliana
tu bila ubishi kuwa burudani huwa haikosekani popote penye uwepo wa mkali
mwenye vipaji rukuki, yani movies, comedy na hata muziki Jamie Foxx. Movie inamhusu mtu mwenye kipaji na ujuzi wa kuendesha gateway “Baby” ambaye amelazimishwa kumtumikia boss mharifu.
Nisiharibu utamu, tafadhari itazame na hutojutia hata sekunde yako moja.
6.
John Wick Chapter 2.
Iwapo wewe ni mdau wa
action movies za kigumugumu na haukuiona John
Wick ya kwanza, inakubidi uharakishe kuitafuta kabla hujaitazama hii. Movie
hii imefanikiwa kupasua miamba kwa matukio ya action zake, humo kuna mitupo ya
hatari ya risasi ya kiwango cha kurarua mataya, mambo ya Keanu Reeves muuaji anayevaa
nadhifu muda wote.
7.
Wonder Woman.
Movie hii inamhusu mtu mmoja jasiri sana
anayekabiliana usumbufu wa hapa na pale. Kila kitu kinakwenda safi kuanzia
mwanzo mpaka mwisho anapoamua kupambana na hatimaye kumshinda mtu mbaya sana
(adui kuu). Sote tunapenda kutazama movie nzuri ambazo ndani yake zina mwanamke
kama mhusika mkuu.
8. Dunkirk.
Je, wewe huwa unapenda kutazama
movie za kivita? Hapa ndo pahala pako sahihi pa kuketi. Dunkirk mpambano mkali
unaotokana na muunganiko wa wanajeshi kutoka Ubelgiji, falme ya Kiingereza na wengine kutoka Ufaransa wanazingirwa na
jeshi la Ujerumani wakati wa Vita Vya Dunia II na hatimaye wanaokelewa.
9. Kong:
Skul Island.
Wanasayansi na
adventures kwa pamoja na kikosi cha jeshi wanaungana kwenda kuona kile
kinachosadikika kuwamo kwenye kisiwa kilichopo Bahari ya Pasifiki. Baada ya
kupekuapekua hapa na pale na kukanyaga hili na lile wanajikuta uso kwa uso na Kong, sasa
jiweke sawa kuona mpambano wa binadamu na asili ya kisiwa hicho.










No comments:
Post a Comment