Ni nini ambacho bado
hujasikia kuhusu bondia huyu bora kabisa aliyepata kutokea duniani?
Mbabe huyu mwenye miaka
50 anafahamika vyema karibu na kila mtu kama mwamba wa ngumi za uzito wa juu,
na ile tattoo yake ya jichoni. Pia kwasasa anafahamika kupitia tasnia ya filamu
na anaeleweka kuwa si mtu wa kubishana naye hovyo hovyo. Mbali ya haya yote
ikumbukwe kuwa mwamba huyu ameshahusika kwenye matukio mengine ambayo ni ya
ajabu sana kwa mtu mwenye akili timamu akiyatafakari.
Swali langu ni je, unapata
taswira gani unapomfikiria Mike Tyson? Kwamba ni mtu wa aina gani kwenye
kujenga hoja?
Anavutia, mpole, mcheshi? Sahau namna yoyote ufikiriavyo kuhusu Tyson alivyo.
Hamishia akili yako hapa na upate simulizi za kweli kumhusu na mambo kadhaa
aliyopata kuyapitia maishani mwake.
Katika Makala moja ya New York Magazine, Mike Tyson alisema
hivi kuhusu maisha yake ya awali.
“Kuna watu wanaweza kusoma mambo ninayozungumza na wakanihukumu kama mtu
mzima, wacha tu niitwe mharifu, lakini ikumbukwe kuwa mambo hayo niliyafanya
miaka 36 iliyopita. Nilikuwa bado mtoto mdogo na nilikuwa natafuta upendo ambao
sikuupata sehemu nyingine zaidi ya mitaani. Mtaa ndiyo ulikuwa elimu yangu
pekee na watu wa mtaani ndiyo walikuwa walimu wangu.”
Kwa jinsi Tyson
alivyozidi kukuwa, hakika akapevuka na kuwa binadamu wa namna yake duniani.
Je, ni kwamba Tyson
alijihusisha na maovu katika maisha yake, au ni kwakuwa alizungukwa na
mazingira yaliyomlazimu kufanya uovu? Hili ndilo linazua mjadala mzito, au
tuseme kwamba watu aliokuwa anashinda nao muda mwingi na matendo yake ndiyo
yalipelekea yeye kuwa hivi alivyokuwa. Au ni makosa yake mwenyewe?
Weka akilini mwako
mbali ya kwamba simulizi hii imebeba matukio mengine ambayo ni ya ajabu kueleza,
lakini ni ukweli kutoka kwa Mike Tyson mwenyewe.
15. Tyson Anamshambulia
Mbeba Takataka
Wakati akiwa bado
mdogo, Tyson alikuwa na afya njema, mwenye nguvu
sana na mbabe. Kuna siku alimwona mbeba takataka akiweka mzoga wa njiwa (Tyson alimpenda
sana njiwa huyo) kwenye pipa. Tyson alimfuata na kumtandika ngumi kali kwa
mkono wa kulia iliyompeleka mtu huyo chini na kuumia sana. Yeye alitaka
kumuhifadhi njiwa huyo kwenye boksi zuri kama sehemu ya heshima na upendo.
Tyson anasimulia.
“Niliacha ile boksi kwenye tundu ya kufugia njiwa na
nikaingia ndani kufuata kitu fulani niliporudi nikaona mtu wa takataka anatia
ile boksi yangu kwenye crusher na kuondoka zake. Nilimkimbilia kadiri alivyokuwa anatokomea kuelekea kwenye hekalu moja, kwa
mkono wa kulia nilimchapa konde takatifu akaanguka chini na kuanza kutapatapa
kama kitoto kichanga kinavyojikongoja.”
Cha ajabu mwaka 1996 Tyson
alisimulia tukio hili kwa kujiamini kabisa kanakwamba alifanya tukio sahihi na lenye maadili.
14. Miaka Mitano Bila
kushiriki Ngono
Ni kweli kwamba Mike
“Iron” Tyson kitendo cha ngono mwaka 1981 – 1986.
Alichukua maamuzi ya
kuelekeza akili na nguvu kwenye mchezo wa masumbwi ili awe bondia bora kabisa
ambaye hajapata kutokea duniani, kwahiyo hakutaka kukumbana na kizuizi chochote
njiani. Kwa namna fulani alifikiri kwamba kushiriki ngono kungemfanya awe
dhaifu. Ni hadithi ya wake wa kale kwamba kushiriki kitendo cha ngono kabla
kupigana hushusha kiwango cha testosterone mwilini mwa mwanaume na hivyo kuwa
dhaifu.
Tyson ni mwanaume
mwenye mbinu za kipekee, na huwia vigumu kuuliza mikakati ya ushindi wake wote
alioupata.
13. Kilevi Wakati wa
Mpambano
Wakati wa mpambano wake
dhidi ya Lou Savarese, mwezi june mwaka 2000, Tyson alipigana huku akiwa
amelewa bangi na cocaine kwa wingi na bado aliweza kushinda. Aliweza kukwepa
vipimo kwa kuwasilisha sampuli ya mkojo ya uongo. Anasema kwamba amepigana
mapambano mengi tu akiwa amelewa na mengine hawezi kuyakumbuka.
Cha ajabu zaidi huo
ndiyo ulikuwa mpambano wake wa kurejea kazini na kumuimarisha kama mtu makini kabisa
ulingoni, na kama kuna mtu anayeweza kupigana ulingoni akiwa tilalila basi huyo
Mike Tyson pekee.
12. Mkojo Feki Kwenye
Kipimo Cha Matumizi ya Dawa
![]() |
| Mike Tyson na promota Frank Warren |
Katika wasifu wa Mike
Tyson anaeleza mbinu zake za kukwepa vipimo vya dawa mwilin. Anasema kuwa alitumia
uume wa uwongo uliojazwa mkojo wakati wa vipimo. Tyson anadai mwaka 2000 wakati
wa mpambano wake THC alikutwa na kiwango cha dawa mwilini, kwasabuabu mtu
aliyepewa jukumu la kubeba ule uume bandia alisahau siku hiyo.
Promota wa mapambano
mengi ya Tyson, bwana Frank Warren, anadai kuchukizwa sana na simulizi hizi.
“Nachukizwa sana na
hadithi hizi za kupuuzi, alipopigana hapa alifanyiwa vipimo na UK Sport, ambao
hufanya vipimo vyote vya mabondia na hakuna chochote kilichoonekana kwenye
mfumo wake wake wa damu.” Anasema bwana Warren".
Anaendelea kusema kuwa
haiwezi kuwa kweli bali Mike Tyson anayasema haya ili kuuza kitabu”.
11. Anamtandika Makonde
Don King
Mike Tyson na promota
wake Don King hawakuwa sawa kama vile unaweza kudhani. Mwaka 2003 Tyson aliruka
na ndege yake binafsi kwenda Miami – Florida kuonana na King. Tyson akaanza
kumkong’ota ngumi na makonzi King aliyekuwa akiendesha gari kuelekea sehemu
fulani kufanya mazungumzo yao.
Tyson anakiri kuwa
walikuwa na mahusiano mazuri na King. Lakini alimchukia tu kwasababu ambayo
bado hajaiweka wazi lakini inawezekana sababu ikawa ni zile $400 mil ambazo
zilitoweka ghafla uweponi mwa Tyson.
Hata hivyo tuelewe tu
kuwa kupigwa kichwani na mtu kama Tyson maumivu yake si madogo, mbali ya hayo,
hakika akikukong’ota sehemu yoyote mwilini ni lazima uugulie kwa sana.
10. Amtundika Mimba
Afisa wa Gereza
Ndani ya gereza kuna
umm, upuuzi mwingi tu hutokea humo. Tyson alikuwa alipangiwa kuonana na mshauri
(counselor) wa gereza mara moja kila juma, na hatimaye akawa na mahusiano ya
kingono mara tatu kwa siku. Mambo yakaendelea kuwa hivyo mwishowe yule afisa
akashika mimba, Tyson ananukuliwa akisema “nilimpa mimba afisa jela nilipofungwa
gerezani, lakini hakupata mtoto.”
Tyson anaendelea kusema
kwamba mambo haya yanatokea sana gerezani kama kitu cha kawaida. Lakini hili si
jambo linalofanya watu watafakari sana juu ya tabia yake, isipokuwa ni juu ya
maadili yake na ni nani aliyemfunza maadili hayo? Huyu ndiyo Tyson, hakika
hakufunzwa na mtu bali alijifunza mwenyewe hata angali mtoto mdogo kabisa.
9. Mitch Green
Mwaka 1988, Mitch
Green, bondia wa uzani wa juu alikutana na Tyson kwenye kituo cha biashara
(shopping mall). Green alishatwangwa na Tyson kwenye mpambano kwahiyo akasema
anataka mpambano mwingine. Lakini badala ya kufanya makubaliano ya tarehe ya mpambano
Tyson akaanza kumtandika Green hadharani, bila kujali kuwa Green alikuwa bado
anamajeraha kadhaa mwilini. Green ndiye aliyeanza kumkabili Tyson kwasababu
alidai kuwa Don King bado hajalimpa stahiki zake za mpambano wao wa kwanza. Hatimaye
mahakama ya kiraia ikaamuru Tyson kumlipa Mitch Green kiasi cha $45,000 kwa
madhara ya kushambulia hadharani.
Pamoja na kwamba Tyson
alimshushia kipigo kizito bondoa huyo na kumwonyesha huo ndiyo mpambano wa
marudiano aliouhitaji kwa kumchakaza uraini. Kipigo hicho cha mbwa mwizi
kilipelekea macho ya bwana Green kuvilia damu na kusababisha asiweze kuyafungua
tena.
8. Hongo kwa Afisa wa
Zoo
Mwaka 1989 tyson
alianikiwa kumhonga mtunza bustani ya wanyama na kuachiwa atembee bustanini
humo kwa saa kadhaa akiambatana na mkewe. Alikuwa eneo la masokwe Mike Tyson
alijaribu kumhonga mtunza bustani hiyo kiasi cha $10,000 ili asizuiwe kwenda
kuingia kwenye cage akapigane na sokwe aliyekuwa anamshambulia mwenzie. Shukurani
kwa huyo mtunza bustani kwani alikataa kumruhusu Tyson asije raruriwa na mnyama
huyo mwenye ghadhabu. Ubabe wake ni kwa binadamu wenzie tu na siyo wanyama
wakubwa kama sokwe hahahahaaa…..hao ni viumbe wengine kabisa.
Mtunza bustani
alishafanya kosa kumruhusu Tyson kuzurura bustanini humo na kamwe hakutaka tena
kurudia kosa kwa kumwachia akapigane na mnyama.
7. Akong’ota Washabiki
Wake
Mike Tyson anadai kuwa
ananmna yake ya kukabiliana na washabiki wake. Hata wale waliomba saini yake. Tyson
anakiri amewahi kuwatandika makonzi na makofi mashabiki wake waliozidisha midadi.
Mwaka 2003, Tyson
alivamiwa ghafla na washabiki wawili kwenye lango kuu la hoteli anadai kwa kuendeshwa na akili ya ulevi wa cocaine aliwakimbiza akamchapa mmoja
konde la uso lilipelekea kupoteza fahamu, na yule mwingine akaokolewa na
mtumishi wa hotelini hapo baada ya kutoa taarifa kwa walinzi.
Hii ndiyo tabia ya
Tyson ni mkorofi na humshambulia mtu yeyote anayemsababishia usumbufu.
6. Awekewa Bastola
Kichwani
Mwaka 1983, Tyson
alikuwa bado yuko kwenye rika la balehe, mwalimu wake Teddy Atlas alimwekea
bastola kwenye paji la uso. Atlas alidhani kwamba Tyson alikuwa na mahusiano ya
kingono na binti yake wa miaka 11, akamuonya Tyson kuwa asijaribu kucheza na
familia yake au la atakufa. Teddy akafutwa kwenye chama cha ngumi cha Catskill
baada ya tukio hili.
Baada ya siku kadhaa
Tyson alidai kuwa aliwahi kushika makalio ya binti yake Yeddy mara moja. Tyson huwa
hakatai jambo ambalo amelifanya, lakini aliingiwa na woga baada mzee huyo wa
kizungu kumwelekezea bastola ile kichwani, hasa ukizingatia wakati huo kesi ya
ubaguzi wa rangi ilikuwa imeshika moto nchini humo.
Teddy akaendelea
kuwafundisha mabondia wengine na akawa mtangazaji wa michezo. Sidhani kama
baada ya hapa Tyson na Teddy walichekeana tena, hapana siyo rahisi kabisa.
5. Miujiza na Uchawi
April 1, 1992 wakati
Tyson akiwa gerezani kutumikia adhabu yake ya kesi ya ubakaji, alijaribu
kutafuta mbinu mbalimbali za kupunguza kifungo chake. Tyson alimsikiliza mchawi
mmoja na akafanya mambo fulani kufuatisha maelekezo. Akaweka $500 mtungi wa
glasi (sifahamu aliutoa wapi wakati akiwa humo ndani), akakojoa humo na kuosha
mikono yake kwa kutumia mafuta ya aina mbalimbali na maji. Pia akanywa kinyaji
cha detox baada ya kufuatisha maelekezo yote ya awali ya uchawi huo.
Pia alifanya uchawi
mwingine wa kutupa yai sakafuni na kupiga uyowe huku akitamka neno “I’m free”. Nadhani kuanguka na kupasuka
kwa yai kuliashiria kuwa Tyson kutoka kwake gerezani miaka mitatu baadaye. Huenda
ni kweli ulozi huu ulikuwa ni sehemu muhimu ya kuachiwa kwake huru, hakuna
ajuaye!!!!!
4. Alipowehuka akiwa na
Steve-O
Bila shaka sasa
umetambua kwamba Mike Tyson alikuwa mpenzi sana wa kubwia unga. Wakati wa
intavyuu moja na GQ alifinguka kuwa dawa za kulevya zilichochea kukuwa kwa urafiki
baina yake na huyu bingwa wa ngumi mstaafu. Unaweza usiamini ukiambiwa kuwa hawa
jamaa walijifungia bafuni na wakabwia cocaine gramu 5.5. na kali zaidi ni pale
Tyson alipoamua kutoa tumbaku yote kwenye sigara na kuijaza cocaine. Ingawa walikuwa
pamoja humo bafuni lakini alitumia cocaine yote peke yake.
3. Akiri Kufanya Maovu
ya Zaidi ya Ubakaji
Mwaka 1991, Tyson
alidai kwamba katika maisha yaake ameshafanya mambo matano–saba ambayo ni maovu
zaidi ya kumbaka mtu.
Inawezekana vipi
kufanya mambo hayo matano mpaka saba ambayo ni mazito zaidi ya ubakaji? Kuna jambo
gani lingine ambalo ni zito zaidi ya hilo? Labda tuseme kuua mtu ni tukio baya
na zito zaidi, au labda kuiba mwili wa marehemu. Kwakweli hili ni japo la
hatari sana ambalo halifai hata kulijadili.
Mara kadhaa
ameshaliongea hili kwamba ni kweli mambo mengi maovu sana na hajawahi kuonekana
kujutia lolote. Hata kama anaonyesha kusikitishwa na matukio hayo hautaweza
kuamini kuwa anayesimulia ndiyo mtenda maovu hayo. Si jambo rahisi mtu kusema
kuwa umembaka mtu fulani, kumbaka mtu ni jambo la hatari na haipendezi mtu
kuutenda uovu huo.
2. Awatandika
Machangudoa Saba
Mwaka 2009, Tyson
aliwazabua machangudoa; siyo mmoja ama wawili, alitandika makofi wadada saba. Alikuwa
amelewa usiku huo, kama watu wengine na akawa kama kavurugwa akili.
Alikuwa amejipigilia morphine, cocaine na akashusha na vodka. Akadhani madada
poa wangeweza mchomolea wallet yake, kwahiyo akang’aka.
“Nilikuwa nipo sehemu yenye giza. Kulikuwa kuna namna ya ujanja
nilidhani nafanyiwa, kwasababu kuwaachia hata senti moja” anasimulia Tyson.
Maelezo yake yanafanya
aonekane mwehu. Mbali ya kuwashambulia wanawake hao saba na kuwatoa na damu na pia
kuwaachia makovu, anadai kwamba siku hiyo alikumbana na shetani halisi katika
mwake akidai kuwa majini na maruhani yanamuwinda sana.
1.
Brad Pitt vs Mike Tyson
Mwaka 1988, kuna siku
Tyson alikuwa anenda nyumbani kwa mtalaka wake bila kumtaarifu. Akiwa anaendesha
taratibu kuelekea kwenye parking ya Robin Givens, akaona hakukuwa na gari hivyo
akilini mwake akajua hapakuwa na mtu pale nyumbani.
Akatembea mpaka
mlangoni akasimama kwa mkono ukiwa kwenye kengele ya mlango, akashtushwa na
muungurumo wa gari kabla hajapiga hatua ya kuondoka eneo lile, alipoitaza
parking akiona gari ya mcheza sinema Brad Pitt akiwa na mkewe Robin. Pitt anasimulia
kwamba hili lilikuwa ni tukio la kutisha sana, alihisi kama amekutana na mzimu.
“Siku moja naenda nyumbani kwake kumsabahi kwa mara nyingine lakini
nyumbani hakukuwa na mtu, sasa natoka naona mtu huyu hapa anakokotana Brad Pitt
wakirejea, nilipatwa na uchungu sana. Wakati huo hakuwa Brad Pitt huyu ……kalikuwa
ni kabichi fulani tu…..nikamtazama tu, alikuwa anautumia mwili wake kujipatia
kipato au kitu fulani, mi sielewi……..lakini tambua tu kuwa jamaa kalikuwa
kazurizuri hivi.” Anasimulia Tyson.
Cha ajabu Tyson
hakumshambulia Pitt, alijivuta taratibu na kuondoka nyumbani kwa Robin. Haijafahamika
mpaka sasa kwanini Pitt hakukong’otwa kama watu wengine waliojileta kwenye uso wa
chuma “Mike Tyson”.
Makala hii
imetafasiriwa na Davis Mwakalosi kwa hisani ya jarida la The Sportster la
Marekani, unaweza kuwasiliana na mwandishi huyu kwa email sportstz17@gmail.com
















No comments:
Post a Comment