Ni mtoto mkubwa wa kiume wa Alpharita Constantia Anderson "Rita Marley", na hayati Robert Nesta Marley almaarufu Bob Marley mfalme wa muziki wa rege duniani.
![]() |
| Kushoto: David Nesta Marley "Ziggy akiwa na baba yake, hayati Robert Nesta Marley "Bob" mwaka 1973 |
![]() |
| Ziggy (katikati) akiwa na wazazi wake pamoja na ndugu zake Cidella (kushoto) na Sharon (kulia) na Stephen (kwenye kiti mwaka 1973. |
Alipozaliwa mnano October 7, 1968 mjini Kingston Jamaica wazazi wake walimpatia jina la David, alijiita Ziggy ambayo ni kifupisho cha jina la Kijerumani "Sigmin au Ziegenbein" ambalo hupewa mtoto wa kiume likimaanisha ulinzi kuelekea ushindi. Maisha yake ya awali wakati wa makuzi yalikuwa kwenye kitongoji cha Trench Town, ni moja ya maeneo wanaishi watu masikini sana wakati huo baba yake alikuwa bado anapambana kuikuza bendi yake The Wailers (ambayo baadaye ilipata kufahamika kama Bob Marley & The Wailers). Inafahamika kwamba hata mama yake Rita Marley ni muimbaji pia naye alijiunga na bendi hiyo katikati ya miaka ya 1970.
![]() |
| David Nesta Marley miaka ya 80 |
Kwa juhudi yake binafsi amefanikiwa kuifanya familia ya hayati Marley kuendelea kuwa ya muziki siku zote hata baada ya baba yake kufariki yeye akiwa bado ni kijana mdogo sana, amelifanya jina liwe miongoni mwa wanamuziki maarufu wa rege duniani.
Wakati akiwa bado mtoto mdogo chini ya miaka minne familia yake ilihama kutoka Trench Town na kwenda kuishi eneo lingine la Wilmington Delaware ambako mdogo wanayefuatana Stephen alizaliwa mwaka 1972.
Lakini wakati huo walikuwa tayari wanna dada yao mkubwa anayefahamika kwa jina la Cedella na dada yao Sharon ambaye Rita alimpata kabla hajaoana na Bob Marley. watoto hawa wanne kwa pamoja walifanikiwa kurekodi wimbo wao wa kwanza "Children Playing in the Streets" mwaka 1979. Wimbo huu uliandikwa na baba yao na ulizungumzia maisha masikini wanayoishi watoto nchini Jamaica. Na mapato ya wimbo yalitumika kama mchango kwenye mfuko wa watoto wa umoja wa mataifa (UNICEF).
The Melody Makers
Baada ya kifo cha baba yake, Ziggy aliimba pamoja na Stephen kwenye mazishi. Kwahiyo baadaye wakaendelea na harakati za kimuziki na kuunda bendi ya The Melody Makers wakiwa na Sharon na Cidella. Wote wanne walikuwa waimbaji lakini Ziggy Marley alipiga gita, chombo ambacho alifundishwa na baba yake, Stephen alipiga gita pia pamoja na ngoma (drums). Melody Makers waliachia wimbo wao wa pili "What a Plot" mwaka 1981.
Na mnamo mwaka 1985, The Melody Makers walifanikiwa kuitambulisha santuri (album) yao kwanza sokoni "Play the Game Right", ambayo haikuwa na mafanikio sana. Juhudi zao wakaelekeza kwenye "Hey World", album yao ya pili mwaka 1986 ambayo pia ilitumbukia kwenye shimo la bahati mbaya kama ile ya awali.
Album iliyotoboa
Walibadili jina na kundi likafahamika kama Ziggy Marley & The Melody Makers kisha wakaachia album yao matata sana "Conscious Party" mwaka 1989 kwenye studio za Virgin Records. Album ilifanikiwa na kulisaidia kundi kujipatia washabiki wengi sana. Ilihaririwa na producer Chris Frantz pamoja na Tina Weymouth wa bendi ya Talking Heads, ilichanganya vionjo vya muziki wa rege, pop na rock. Nyingi ya nyimbo ziliandikwa na Ziggy, alifanikiwa kuandika "Tomorrow People" wimbo usiochosha masikio ya msikilizaji na utaendelea kudumu kwa muda mrefu sana, album ilifanya vizuri kwenye pande zote za muziki wa pop na R&B/hip-hop charts nchini Marekani. Na mapema mwaka 1989 bendi ikatwaa tuzo ya Grammy kama album bora ya rege.
![]() |
| Ziggy Marley akiwa kwenye Tamasha la Bob Marley 2005 |
Bendi iliendelea kufyatua kadhaa kwa pamoja miaka ya 90, ikiwemo kujishindia tuzo ya Grammy kwa album yao ya "Fallen Is Babylon" mwaka 1997 kabla bendi haijasambaratika.
Mafanikio binafsi
Kwa kuangazia jamii, siasa na mambo binafsi, Ziggy alifyatua album yake ya kwanza "Dragonfly" mwaka 2003. aliwashirikisha watu kadhaa akiwemo Flea na John Frusciante kutoka kundi la Red Hot Chili Pappers, album yote ilikuwa katika mfumo wa rock na hip-hop. Jitihada yake hatimaye ikafinikiwa kuleta "Love Is My Religion" mwaka 2006 na kuibuka kinara kwenye tuzo za Grammy kama album bora ya rege.
Marley aliendelea kufanya muziki mzuri kama kawaida akiwa kama mwanamuziki anayejitegemea na pia akiwa na ndugu zake na hata wanamuziki wengine maarufu duniani akiwemo Donna Summer. Album aliyoiita "2016" ilibeba tuzo ya album bora ya rege na hivyo kumfanya kuwa na jumla ya tuzo saba za Grammy.
Pia kupitia kazi yake ya muziki, ameunda kitu kinaitwa U.R.G.E (Unlimited Resource Giving Enlightment) shirika linalosaidia watoto walio katika dimbwi la umasikini. Anawatoto wanne na mkewe Orly Agai.
![]() |
| Ziggy na familia yake wanapata chakula pamoja |
Na inakadiriwa kuwa Ziggy Marley anautajiri usiopungua dola za marekani milioni kumi.
![]() |
| Ziggy Marley akiimba na mama yake miaka ya hivi karibuni |
(Makala hii imetafasiriwa na Davis Mwakalosi kwa hisani ya mtandao wa www.bibliography.com )







Anahistoria ndefu ya muziki aisee
ReplyDeleteHata his music carries strong messages
Delete