![]() |
| Floyd "Money" Mayweather katika moja ya mapambano yake. |
Jumapili ya Agost 27,
2017 Floyd Mayweather alishinda mpambano uliobatizwa jina la Pigano la Pesa
“The Money Fight” na sasa ameingia kwenye uwanja mpya wa klabu ya wanamichezo
mabilionea “The Billionaire Athlete Club” kwa thamani ya dola ya Marekani.
Mayweather anatarajia
kuweka kibindoni kiasi cha $300 milioni kutoka kwenye mpambano wake dhidi ya
Conor McGregor, mkali wa mchezo wa mapigano mchanganyiko (MMA) aliyechakazwa
raundi ya kumi ya mpambano huo. Pesa hii ikithaminishwa kwa Shilingi ya
kitanzania tarakimu yake inasomeka ni 672,300,000,000.00, yaani bilioni mia
sita sabini na mbili na milioni mia tatu.
![]() |
| Floyd Mayweather vs Conor McGregor kwenye mpambano wa pesa Agosti 27, 2017. |
Bondia huyu mwenye mbwembwe nyingi sasa anajivunia rekodi yake ya kushinda michezo 50-0, ameshajikusanyia jumla ya
$700 milioni kutokana na kazi yake hii ikiwemo malipo ya haki za matangazo ya
televisheni, mauzo ya tiketi na malipo ya kupigana ulingoni.
Leonard Ellerbe,
promota mkuu wa Mayweathe anasema “baada ya pambano hili, Mayweather anaungana
na mkali wa basketball Michael Jackson na mwamba wa mchezo wa golf Tiger Woods
na kuwa ni wanamichezo watatu pekee waliofanikiwa kujitengenezea kiasi cha pesa
kisichopungua $1 bilioni.
“Sidhani kama amewahi
kuikosea kazi yake,” aliongeza Ellerbe.
Jordan alitengeneza
zaidi ya $93 milioni kwa kazi yake, kulingana na maelezo ya kampuni ya Spotrac
ya utafiti wa mishahara. Hata hivyo bado anamikataba mingine kadhaa ikiwemo ule
wa kudumu na kampuni ya Nike.
Mikataba hii imemuwezesha
kuingia kwenye kilabu cha mabilionea, na hata
umiliki wake wa Charlotte Hornets (klabu ya mpira wa kikapu USA). Mwaka
2015 kwa mara ya kwanza aliorodheshwa miongoni mwa mabilionea kwenye gazeti la
Forbes.
Tiger Woods pia aliwahi kuwemo kwenye orodha
hiyo. Mwaka 2009 Forbes ilikadiria kuwa ushindi na mikataba yake mingi
inamfanya Woods kuwa bilionea. Lakini akiba yake kwa miaka ya hivi karibuni
imeporomoka kwakuwa hajaweza kushinda mashindano yoyote tangia mwaka 2008.
Na ile kashfa kubwa ya kingono imesababisha wadhamini kumtema. Forbe inakadiria kuwa utajiri wa Woods kiasi $740 milioni mwaka 2016.
Mwanamichezo mwingine
anayenekana kuelekea huko pia ni LeBron James. Nyota huyu wa kikapu (NBA)
anamwelekeo mzuri ameshajipatia mamilion ya dola kazi yake kama mchezaji na
kusaini mikataba mbalimbali ikiwemo ule wa kudumu na kampuni ya Nike tangu
mwaka 2015.
![]() |
| Mayweather akiwa katika pozi kwenye gari lake la thamani kubwa |



Go Floyd, hit dem fool heads
ReplyDelete