Na Davis Mwakalosi
Alexis Sanchez na Mesut
Ozil inawezekana wakatembea zao mwakani, na pia Aaron Ramsey na mapanki Danny
Welbeck wakaondoka msimu unaokuja.
![]() |
| Ramsey na Welbeck wakati wa mazoezi eneo la uwanja wa timu yao ya Arsenal |
Bila kujali kwamba
mikataba ya Welbeck na Ramsey inaelekea ukingoni mzee Wenger bado
amesimamia msimamo uleule wa kutokubadili sera za mikataba ya klabu yake ya
Arsenal.
Arsenal wajiandae tu kisaikolojia kuwaachia Ozil na Sanchez kwakuwa wote wawili mikataba yao inafika ukomo ndani ya muda mfupi ujao hivyo kunauwezekano mkubwa wakaondoka na klabu isiambulie hata senti.
Mwingine ni Jack Wilshere ambaye amebakiza chini ya mwaka mmoja, ikumbukwe kuwa Alex Oxlade Chamberlain aliuzwa kwenda Liverpool fc akiwa amebakiza miezi 12 tu kumaliza mkataba na Arsenal.
![]() |
| Arsenal fc wanaonyesha dhahiri watakosa huduma ya Sanchez na Ozil msimu ujao bila ya kuambulia hata senti moja. |
Jirani zao, yaani
Tottenham Hotspurs wameshapata somo na sasa wamekuwa macho kutokuruhusu
mikataba ielee elee chini ya miaka miwili, hawatasau maumivu ya kumpoteza beki kisiki Sol Campbell aliyeondoka
bure kuelekea Kaskazini mwa London kwa mpinzani wao mkubwa Arsenal mwaka 2001.
Ramsey na Welbeck wote wana miaka 26 na wamebakiza mikataba ya miaka miwili.
Ramsey analipwa pound
100,000 kwa wiki, alifunga bao la ushindi wa fainali za kombe la FA mwezi May na
bado ni mchezaji muhimu sana kwenye kikosi cha kwanza cha Arsene Wenger.
Welbeck amepambana na majeraha yalimuweka nje muda mrefu na kufanikiwa kujiimarisha miongoni mwa wachezaji muhimu wa kilabu hiyo. Mmshambuliaji huyu wa kiingereza analipwa pound 70,000 kwa wiki atakuwa nje ya uwanja hadi October kutokana na jeraha la kinena alilopata wiki iliyopita kwenye michuano ya kimataifa.
Wenger anasisitiza kuwa hana hofu baada ya kina Sanchez kuwa katika mpango wa kuongezewa mikataba yao bila kuifanyia mabadiliko ya kisera.
“Hakuna kabisa”
aliongea kuelekea mchezo wao wa jumatatu dhidi ya West Brom. “Kiasi cha pesa
cha uhamisho na kile cha mkataba anachotaka mchezaji, utaona ni wachezaji wengi
wapo kwenye mwaka wa mwisho mikataba yao.”
“Kwahiyo utajikuta upo
kwenye sehemu ambayo inatakiwa uongeze mkataba usioumudu malipo yake au la utaacha
tu mwaka umalizike.” Alisema Arsene Wenger.



No comments:
Post a Comment