MATUKIO 25 YA KUFURAHISHA AMBAYO HUKUWAHI KUYAFAHAMU KATIKA MIAKA 25 YA EPL - SPORTSTAIN

SPORTSTAIN

Stay with us. Be informed

Sunday, 24 September 2017

MATUKIO 25 YA KUFURAHISHA AMBAYO HUKUWAHI KUYAFAHAMU KATIKA MIAKA 25 YA EPL

Na Davis Mwakalosi

Miaka 25 baada ya kuundwa kwa ligi kuu Wingereza (English Premier Leagu), huu ni mzigo kamili wa matukio ya ajabu yaliyotokea ambayo kwa hakika hukuwahi kuyafikiria  wala kuyasikia kabla ya leo.
Hii ndiyo Ligi yenye umaarufu kushinda zote duniani

01.Ni wachezaji wawili tu waliofunga penati kwa miguu kwa miguu yote miwili, Bobby Zamora na Obafemi Martins.
Bobby Zamora

02.Ryan Giggs ndiye mchezaji aliyefanyiwa sub nyingi kuliko mwingine yeyote, (134).
Ndiyo ni kweli hatuwezi kukataa kwamaba amecheza michezo mingi kwakuwa ametumia muda wake wote EPL, lakini amejiongezea rekodi yake nyingine ambayo ni hii.

03.Mario Baloteli amepiga pasi ya goli moja tu kwa Sergio Aguero kwenye EPL katika mchezo baina ya Man City na Queens Park Rangers.
Sahau habari ya Man City kunyakuwa ubingwa wa ligi msimu huo, lakini ukumbuke tu ya kwamba bao hili la Sergio Aguero kwenye mchezo dhidi ya QPR lilitokana na pasi ya Mario Baloteli.

04.Wayne Rooney, Gareth Bale na Kevin Davies ni wachezaji pekee waliofunga, kutoa pasi ya goli na kujinga katika mchezo mmoja.
Wayne Rooney akijifunga kwenye mchezo wa Man U dhidi ya Stoke City mwaka 2012

05.Man U ni klabu ambayo haijapoteza mchezo Old Trafford baada kuongoza kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
Sir Alex Ferguson, shukurani nyingi ziende mzee huyu mwenye rekodi kibao kwenye timu hiyo

06.Alan Shearer amekosa penati nyingi zaidi kwenye EPL (11), lakini pia ndiye aliyfunga nyingi kuliko wote (56).
Alan Shearer akishangilia bao msimu wa 2002/03

07.Msimu wa 2015/16 ilikuwa ni mara ya kwanza kwa West Ham kufunga magoli mengi kuliko msimu wa 1985/86.
Msimu wa 2015/16 ulikuwa ni mzuri kwa West Ham kiasi cha kufungua shampeni na kulipua mafashifashi 

08.Kipa mstaafu wa timu ya taifa ya Wingereza Paul Robinson, ameshafunga, ametoa pasi ya mwisho na kufunga penati kwenye EPL. Ndiye mwenye pasi za mwisho (5) nyingi kuliko golikipa mwingine yeyote kwenye ligi hiyo.
Paul Robinson

09.James Milner amefunga magoli 47 kwenye EPL na kila anapofunga basi timu yake ya Liverpool haikupoteza mchezo.
James Milner akiwa Liberty Stadium kwenye baina ya Burnley na Liverpool

10.Ni wachezaji watatu pekee waliozaliwa baada ya ligi hiyo kuitwa English Premier League (August1992) wamefanikiwa kupiga hat-tricks, Raheem Sterlin, Harry Keane na Romero Lukaku.
Harry Keane na moja ya mipira yake mingi aliyoipata baada ya mchezo kumalizika

11.Mtu pekee aliyezaliwa kabla ya mwaka 1960 na kufunga hat-trick kwenye English Premier League ni Gordan Strachan.
Raia wa Scotland, Gordon Strachan amezaliwa February 9, 1957 na kuchezea Leeds United na Coventry City baada ya mfumo kubadilishwa na kuitwa English Premier League.

12.David (x14) na James (x11) yalikuwa majina yaliyozoeleka sana kwenye English Premier League msimu wa 2010/11, lakini haikuwa hivyo kwa golikipa David James, kwani hakufanikiwa kucheza hata mchezo mmoja.
David James

13.Msimu wa 2014/14, George Boyd akawa mchezaji wanne kuchezea timu mbili ambazo zote zilishuka daraja kwenye msimu huo huo wa ligi, wengine ni Mark Robins 1994/95, Steve Kabba 2006/07 na David Nuget 2009/10.
George Boyd wakati akiitumikia timu ya Burnley kwenye msimu wao mbovu.

14.Msimu wa 2014/15 Leicester City ilikuwa ni timu iliyokaa mkiani mwa msimamo wa ligi kwa muda mrefu zaidi bila kushuka daraja kuliko katika historia kwa jumla ya siku 142.
Claudio Ranieri

15.Cezar Azpilicueta (2016/17), Wes Morgan (2015/16), John Terry (2014/15) na Garry Pallister (1992/93) ni wachezaji pekee waliocheza dakika zote msimu husika wa ligi na kubeba ubingwa.
John Terry

16.Peter Crouch amefunga mabao mengi kwa kichwa (50) zaidi ya 16 yaliyofungwa na timu alizochezea kwneye English Premier League.
Pic
17.Nuri Sahin (mchezaji wa zamani wa Liverpool) amecheza michezo mingi bila kuwa sub kuliko mchezaja yeyote kwenye michezo ya English Premier League (7).
Peter Crouch akifunga la kichwa dhidi ya Liverpool

18.Richard Wright amecheza michezo 12 tu kwenye Enlgish Premier League, michezo (12) akiwa Arsenal na (0) akiwa Man City, lakini ameshasherehekea ubingwa wa ligi mara mbili.
Richard Write mwenye bahati ya mtende, bahati haba ya kucheza lakini amebeba ubingwa mara mbili.

19.Lago Aspas amepiga mipira mingi ya kona hovyo kuliko akipiga kawaida.
Lago Alpas mfalme wa kona mbovu

20.Msimu wa 1997/98, Andy Roberts alicheza michezo 37 kwenye English Premier League na kati ya hiyo minne aliumana na Arsenal fc (miwili akiwa anaitumikia Crystal Palace na miwili mingine akiwa Wimbledon).

21.Terry Connor, ndiye kocha pekee kwenye English Premier League aliyepata kufundisha vilabu zaidi ya kumi bila kuchukua ubingwa hata mmoja.
Masikini mwe, Terry Connor

22.Msimu wa 2016/17, Hull City imekuwa ni timu ya tatu kuwahi kushika nafasi tatu za juu na msimu huohuo kushuka daraja. Nyingine ni Charlton 1998/99 na Bolton Wanderers 2011/12.
Hull City wakishangilia bao kwenye mchezo dhidi ya Leicester City

23.Ni wachezaji wawili tu waliopiga hat-tricks kwa kichwa kwenye michezo ya English Premier League: Duncan Ferguson wa Everton (dhidi ya Bolton Wanderers, Dec 1997) na Solomon Rondon wa West Bromwich (dhidi ya Swansea Dec 2016).

Solomon Rondon
uchambuzi huu umekujia kwa hisani ya mtandao wa Mirror wa Wingereza

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad