PIA: Gunners wakwazika maamuzi ya FA juu ya tukio la Richarlison.
Arsenal wanaweza
kumsajiri striker wa AC Milan, Andre Silva wakati wa majira ya joto.
Mchezaji huyo wa
kimataifa kutoka Portugal alihusishwa na kwenda Emirates kabla hajakamilisha
uhamisho ulioweka record San Siro.
Dalili hainyeshi
maendeleo mazuri kwa Milan kiuchumi na hata kisoka kiasi kwamba wameanza vibaya kwenye ligi ya klabu bingwa Ulaya.
Kulingana na taarifa ya
The Sun, Silva atakuwa miongoni mwa wachezaji ambao watanyakuliwa na timu
nyingine iwapo Vincenzo Montella atashindwa kuisimamia timu vyema.
![]() |
| Mchezaji wa AC Milan, Andre Silva akiwa kazini. |
Wakati huohuo FA
imethibitisha kwamba mshambuliaji wa Watford, Richarlison hataadhibiwa kwa
udanganyifu uliopelekea kupata penalty iliwapatia ushindi wa 2-1 dhidi ya
Arsenal.
![]() |
| Richarlison anakwenda chini. |
Mbrazil huyo
alijishindia zawadi ya penalty kufuatia kusukumana na mlinzi wa Gunners, Hector
Bellerin kitu ambacho Arsene Wenger ameita ni maamuzi ya kashfa.


No comments:
Post a Comment