Inter Milan waonyesha nia ya kutaka kumchukua, na tayari mkataba wake unaelekea kumalizika mwisho wa msimu huu.
Boss wa Gunners, Arsene
Wenger hatimaye amekiri hadharani kwamba wanalazimika kuwauza Alexis Sanches na
Mesut Ozil kwenye dirisha dogo la January kuliko kuwapoteza wakiwa huru.
Lakini bado wataendelea
kujaribu kumuweka sawa Ozil ambaye wanaona bado wanauwezo wa kumshawishi
aendelee kubaki kwenye uwanja wa Emirate.
Pia imetokea hali ya kukatishwa tamaa kutokana na tabia ya Ozil na hata uwezo wake uwanjani, hasa baada ya
kipigo walichopokea kutoka kwa Watford Jumamosi iliyopita.
Arsenal wameweka mezani
kitita chenye thamani ya £275.000 kama malipo ya wiki kwa Ozil lakini
wakala wa mchezaji huyo ameikataa offer hiyo na kudai £350,000 huku mazungumzo ya pande zote mbili yakiwa bado yanaendelea kufanyika.
![]() |
| Kazi ya Ozil kwa Arsenal inaonekana sasa inaelekea ukingoni. |
![]() |
| Wenger anaonyesha kutaka kuruhusu Ozil aondoke zake January. |
![]() |
| Ozil aliwaka baada ya Arsenal kupoteza mchezo dhidi ya Watford. |
Tatizo walilonalo
Arsenal ni kwamba Manchester City wanashauku ya kumchukua Sanchez lakini
hawajaonyesha nia ya kumhitaji Ozil.
Inter Milan wamekiri
hadharani kwamba nia yao ni kupata saini ya Ozil na ndiyo maana sasa wanahangaikia
suala hili sokoni.
Arsenal wamepata
matokeo mazuri bila ya uwepo wa Ozil na utambulisho wake kwenye mchezo dhidi ya
Watford ilikuwa ni ishara kuonyesha mwongozo na matokeo yake wakapoteza mchezo
huo Vicarage Road.
Hana makali tena na
mapenzi kwa timu kiasi hali hata hali yake kwenye vyumba vya kubadilishia nguo imekuwa
tofauti, hakika siku zake pale Emirates zinaonekana kuhesabika.



No comments:
Post a Comment