Man U yang'ara dhidi ya Spurs: Anthony Martial katokea benchi na kuweka kamba - Mambo 5 ya mchezo huu - SPORTSTAIN

SPORTSTAIN

Stay with us. Be informed

Saturday, 28 October 2017

Man U yang'ara dhidi ya Spurs: Anthony Martial katokea benchi na kuweka kamba - Mambo 5 ya mchezo huu


  • Mfaransa ameingia dakika 20 kabla ya filimbi ya mwisho na shambulio lake likaleta pointi tatu kwa wenyeji.


Goli la kipindi cha pili lililofungwa na Anthony Martial limeisaidia Manchester United kujipatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Tottenham Hotspurs.
Wageni walilazimika kusafiri kuelekea kaskazini bila ya uwepo wa mashine yao ya magoli Harry Kane, anayeuguza jeraha la msuli na Son-min Heung akachukua nafasi.
Pande zote mbili zilikuwa na tahadhari huku wakitumia zaidi mipira mirefu kipindi cha kwanza, huku makipa wote wakiwa wameshughulishwa kwa namna fulani.
United walianza kipindi cha pili kwa mkiki-mkiki wa Henrikh Mkhitaryan aliachia shuti likazuiwa na Hugo Lloris kabla ya Ben Davies hajazuia tena mpira wa rebound wa Marcus Rashford.
Alli na Young wakitunishiana vifua
Lakini wenyeji hatimaye wakauvunja mwamba na shukurani ziende kwa Anthony Martial aliyeingia dakika 20 kabla ya mchezo kumalizika, aliyemalizia vyema mpira aliolishwa na Romelu Lukaku.
Na hizi ni story tano za mchezo huu:
1 Mourinho aleta kicheko cha furaha 
Mourinho akampa nafasi Martial
Mashabiki wa United wakazomea pale Jose Mourinho alipomtoa Marcus Rashford na Anthony Martial akaingia badala yake zikiwa zimebaki dakika 20.
Lakini Martial akaleta furaha baada ya kumalizia vyema mpira toka kwa Lukaku dakika ya 81.
Kuna muda ni vyema kuyaamini maamuzi ya mwalimu, na leo imethibitishwa.  Mabadiko yaliyobezwa yameleta ushindi United.
2 Manchester United walihitaji kichocheo hiki
Rashford akipambana na Alderweireld
United walianza msimu huu kama treni ya umeme, walikuwa na nguvu haswa na walienda kwa hatua za kufyatuka kitu kilichopelekea waonekane kuwa kweli msimu huu wamekuja kugombea ubingwa kwa nguvu zote.
Lakini wiki za hivi karibuni wakaanza kulegalega, nguvu ya ushambuliaji ikasinyaa. Na cha ajabu zaidi walikuwa wanaelekea kwenye mchezo wa tatu mfululizo bila ushindi hadi pale Martial alipoamua isiwe hivyo.
Hali hii ingekuwa endelevu ni mbaya sana kwani inaitoa timu kwenye mbio za ubingwa. Na sasa wamepata kasi mpya itakayowasaidia kukaa kwenye reli sawasawa.
3 Jumamosi nyingine yenye lunch chungu
Pochettino na Mourinho wakiwa wanatoka uwanjani wakati wa mapumziko
Wakati wa mapumziko, Tv ya Manchester United waliita mchezo huu "intense and exciting." Inawezekana michezo ya mida ya lunch Jumamosi imeleta furaha mara chache tofauti na ile ya katikati mwa wiki, isipokuwa ya Jumapili pekee.
Leo imekuwa nzuri kuliko ile ya Anfield lakini haijawa bora kama walivyotumaini. "Tunaweza kuwa na ratiba ya weekend miada ya lunch Jumamosi kwa siku zijazo tafadhari?"
4 Toby Alderweireld ni beki wa kati bora kabisa kwenye EPL
Alderweireld anambana vyema Lukaku
Bila ya kujali ni beki namba 3, 5 au sehemu ya beki 4, beki huyu raia Ubelgiji atatambulika kuwa ndiye beki wa kati bora kabisa.
Alderweireld amepiga vichwa vingi sana, amezuia mipira mingi ya Manchester United iliyotengenezwa kwa lengo la kushambulia. Alikuwa mchezaji bora kwa leo.
5 Tottenham wanaweza bila ya Kane, lakini wanakosa ubora wao
pic Son achukua pahala pa Kane
Walionyesha kuwa wao ni bora zaidi na si timu ya Kane, lakini bila ya uwepo wake mapungufu yanajidhihirisha uwanjani.
Heung-min Son alicheza sehemu ya mbele, Delle Alli akasogea juu kumsaidia, lakini, wakati Spurs wanaonyesha nguvu yao na kuitikisa ngome ya Manchester, walionyesha kuihitaji zaidi huduma ya Harry Kane.

2 comments:

Post Bottom Ad