Mabingwa wa UEFA wameshuka kwa mara ya kwanza uwanja wa Wembley na kusambaratishwa vibaya na kikosi cha maangamizi cha Mauricio Pochettino
“Beware
The Blacklish” ulikuwa ni ujumbe kwa Tottenham Hotspurs kuelekea usiku wa
Jumatano ya jana, baada ya kipigo cha kushtusha alichopokea Real Madrid toka
kwa Ginora weekend iliyopita.
Mabingwa
hawa wa ligi kuu Hispania na Klabu Bingwa Ulaya msimu uliopita waliambulia patupu mchezo wao wa
Jumapili kwenye La Liga.
Walidhamiria
kuutumia vyema usiku wao wa kwanza kabisa kwenye dimba la Wembley nchini
Uingereza lakini haikuweza kuwa kama walivyotaka.
Na
badala yake, kikosi cha Zinedine Zidane kilishindwa kabisa kufurukuta na
hatimaye kuambulia kichapo cha mbwa mdokozi huko kaskazini-magharibi mwa jiji
la London.
![]() |
| Ronaldo alifunga goli lakini timu yake ilipigwa vizuri sana |
![]() |
| Spurs walikuwa hawashikiki |
![]() |
| Namna ubao ulivyokuwa ukisomeka |
Dele
Alli alitumbukia nyavuni mara mbili na Christian Eriksen naye pia akatumbukia
nyavuni na kuwafanya vijana wa Mauricio Pochettino watoke vifua mbele kwa
ushindi wa 3-1, lakini cha zaidi siyo kilichowatokea Real Madrid, hapa
tuangalie namna vyombo vya habari vya Uhispania vinavyolijadili hili la vipigo
viwili kwa Madrid ndani ya siku nne tu…………..Na lawama zinazoelekezwa kwao.
Gazeti
la AS
Kichwa
cha habari: Usiku wa Majinamizi Wembley
AS
waliweka kichwa hiki cha habari kwenye ukurasa wa mbele sambamba na picha ya
walinzi waliochoka kabisa wakingozwa na Sergio Ramos, Nacho na Kipa wao Kiko
Casilla wakati mpira unatinga nyavuni mwao.
Ndani
yake Javier Silles anaandika kwamba kikosi kazi cha Zidane “Hakika
Hakifanyikazi Sawasawa” pande zote sasa zimedhoofu kuanzia ulinzi, viungo na
washambuliaji hawafanyi lolote la maana kwasasa, kitu ambacho kimetafsiriwa
kama kichapo cha maafa kutoka kwa Spurs.
Viungo
wawili machachari Luka Modric na Toni Kroos wamekosolewa sana kwa kupoteza
umiliki wa mipira mara 28 katika eneo lao kiasi kilichopelekea Kroos
kuangushiwa mzigo wa matatizo yanayowakabili Real Madrid kwasasa.
Tomas
Roncero anamlenga Karim Benzema, “mshambuliaji
wa kwanza katika historia ya Real Madrid asiyeonekana kuhitaji kufunga magoli.”
Gazeti
la Mundo Deportivo
Kichwa
cha habari: Mtazamo wa Madrid
Katika
kulichanganua tukio la jana usiku, gazeti hili la Mundo Deportivo lenye makao
yake Barcelona limeandika Los Blancos “sasa wanaporomoka.”
Manuel
Bruna anasema kwamba “Madrid hawana la
kujitetea” na vijana wanaonekana wamechoka, ni Isco peke yake anayeng’ara
kwa kila kitu, na kuongeza kuwa “Pochettino
amemfunza Zidane somo la kiufundi.”
Josep
M. Artells anaandika kwamba “Casemiro
alikuwa amekumbwa na maafa, Kroos ni kama hakuwamo uwanjani na Modric alikuwa
tepetepe…....Pochettino akamkonyeza Florentino akiashiria kuwa wamemmaliza
mpinzani.
Delle
Alli naye alikuwa na njaa kali baada ya kutupia kambani mara mbili, “alisababisha hofu kuu.”
Gazeti
la Marca
Kichwa
cha habari: Piga Alarm Zote
Huku
wakitumia picha kama ile ya gazeti la AS, Marca hawakutumia maneno yenye hisia
kali……walichosema ni “Usifanye Makosa” lakini kinadharia
huu ni ukosoaji, na ndani yake wanasema.
Harry
Kane aliachiwa huru na sifa zimwendee kwa kuyatimiza vyema majukumu yake
yaliyowapatia ushindi mnono nyumbani ingawa hakufunga. “Hivi Real Madrid hawatafuti mchezaji namba 9? Kwasababu baada ya
kumwona Kane, basi watume skauti wao waende pande yoyote ya dunia lakini isiwe
Wembley kwa maana itakuwa ni kupoteza muda na pesa. Harry ni mwanaume wa soka.”
Hugo
Cerezo anaweka wazi kwamba “mchezo mbaya
kabisa katika nyakati hizi za Zidane” na yeye anathibisha kuwa ni Isco pekee
aliyekuwa hai kwenye mchezo huu.” Anaongeza, “kofi la uso haliji kwa mbabe wa Ulaya,lakini ni mchezo wa marudiano bila ya
ushindi kwenye klabu bingwa Ulaya.”
Gazeti
la Sport
Kichwa
cha habari: Hakuna Malengo
Gazeti
hili pia linatokea jijini Barcelona, kwenye picha anaoneka Cristiano Ronaldo
amevurugwa vibaya sana huku mikono yake ikiwa kiunoni na amepoteza nuru ya uso
wake wakati huohuo wanonekana wachezaji wa Spurs wanashangilia kwa furaha pamoja.
“Matatizo yanazidi kuota mizizi kwa Madrid”
anaandika Ivan San Antonio, anyethibitisha kuwa Delle Alli kiungo wa kiingereza
anayekuja na makali mithili ya moto wa kuyeyushia chuma.
Sifa
nyingine anaelekeza kwa wakali hao wa kaskazini mwa London . “Tottenham
walielekeza nguvu yao ya pamoja kwenye mchezo huu mgumu, bila kupumzika,
hawakuwa na muda wa kufikiria wala kuvuta pumzi,” anaongeza “Tottenham kiukweli
walicheza mpira…….lilikuwa jiwe zito kwa Real Madrid.”







No comments:
Post a Comment