Na: Nsaji Lebhi
Mchekeshaji wa Bongo Movie,
Ulimboka Kajumile Mwalulesya maarufu “Uli Senga” analalamikia maendeleo ya
teknolojia kuwa yanatumika kama ngazi ya kurahisisha wizi kazi za wasanii hasa
wa sinema na muziki.
Senga ametoa kilio
chake alipoongea nasi kwa njia ya simu tulipotaka kusikia sababu ya yeye kutoonekana
kwenye mitandao ya kijamii na mambo mengine kadhaa yanayohusu kazi yake ya sanaa
kwa ujumla.
Anasema kuwa hachukii
kuona dunia inabadilika kitenkolojia lakini matumizi yake kwa baadhi ya watu yamekuwa
ya kiujanja sana kiasi cha kuathiri mapato ya wasanii kwa kiwango kikubwa
kwasababu kazi zao zinaibiwa na kuhifadhiwa kisha nakala zinatengezwa na kuuzwa
bei ya chini ambayo mhusika haambulii hata senti ya mauzo hayo.
Senga anasema kuwa
serikali haipaswi kulaumiwa sana kwa hili hata kama zitatengenezwa sheria na kanuni
kali za kusimamia biashara hii, isipokuwa jamii yenyewe ndiyo inapaswa
kubadilika na kuunga mkono kazi zote ili kila mmoja apate kunufaika kwa nafasi yake.
Akiongelea issue ya yeye
kutooneka kwenye mitandao ya kijamii senga anakiri waziwazi kuwa yeye hatumii
na wala hana ujuzi wa kuitumia ila sasa anataka ajifunze kuitumia ili aendane
na kasi ya dunia pamoja na kujiweka karibu na wateja wake.
Anasikitika sana na
haungi mkono tabia ya watu wa Bongo Movie kuwekeana madaraja hasa kitendo cha wasanii wa vichekesho
kugeuzwa kuwa walinzi na wafungua mageti kwenye filamu nyingi, anaeleza kwa
lafudhi ya Kinyakyusa, “sifurahii kabisa
hii hali……….tunatakiwa tushikamane sote, mimi na mdau wangu Pembe tuko pamoja
na nakuhakikishia daima sisi tutafanyakazi pamoja, kuona tunatenganishwa kikazi ni
sawa na kumtoa samaki majini.”

No comments:
Post a Comment