Blue Ivy akiwa sambamba
na wazazi wake pamoja na wadogo zake Rumi na Sir Carter wameonekana kwa ya
kwanza wakiwa kwenye mtoko wa kifamilia.
Ijumaa jioni wazazi
hawa walionekana wakiwa wamewabeba watoto wao huku wakiwa wanaelekea kwenye maegesho ya helikopta mjini New York huku wakiwa wameambatana na walinzi wao, ilivutia sana macho
ya wengi.
![]() |
| Jay Z akiwa amembeba mtoto wake |
![]() |
| Pichani anaonekana Beyonce kwa mara ya kwanza akiwa na mumewe na watoto wake mapacha kwenye mtoko wa kifamilia. |
Mkali wa ngoma ya “Formation”
alikuwa amevalia mavazi yaliyomka mkaa vyema mwilini akiwa amebeba mkoba huku
msaidizi wake akiwa nyuma yake amembeba mmoja wa mapacha kwenye kibebeo maalum
cha watoto.
Jay Z ameeleza sababu
iliyopelekea kuwapa watoto wake mapacha majina ya kipekee .
Pic Beyonce aliweka
picha hii kwenye ukarasa wake wa Instagram siku watoto wake walipotimiza mwaka
mmoja, July 14.
Akizungumza na Rap
Radar jana Ijumaa namna walifikia kuchagua majina ya watoto wao, alisema, “Rumi ni mshairi tunampenda sana, …….tukaona
ni vyema tumwite binti yetu jina hilo.”
Na alipomzungumzia
pacha wa kiume, mzee wa 4:44 akaendelea kusema, “Ukisema Sir ni sawa na kusema mwanaume, kwahiyo amekuja huyu mwanaume…….na
amekuja kiume.”
Jay Z pia hakuacha
kumwongelea binti ya mkubwa “Blue Ivy” namna anavyoghani mashairi ya nyimbo za
album yake ya sasa 4:44.
Anasema, “alivaa headphones akapanda kwneye stuli kasha
akaanza kurap……..nikastaajabu sana, na ninayo video niliyomrekodi kwneye simu
yangu…….dakika tano, dakika tano akifanya mambo yake.


No comments:
Post a Comment