Louis van Gaal
amemzungumzia Jose Mourinho miezi 16 baada ya kung’olewa kwenye kiti cha
umeneja Manchester United.
Mholanzi huyo akabaki
anashangaashangaa alipokutakana uso kwa uso na Mourinho kwenye korido la
Anfield, ambapo Mourinho akatumia nafasi hiyo kumkaribisha glass ya wine baada
ya sare ya bila kufungana na Liverpool fc.
Kutokana na maelezo ya
Van Gaal, ni kwamba Mourinho alimwita boss wake huyo wa zamani “mister” na akajitahidi kuwa mwema kwake kadiri
awezavyo.
Van Gaal anaamini kuwa
bwana mdogo huyo wa kireno alikuwa anataka sana kupata kazi United hata angali
yeye amekalia kiti cha ukuu pale Old Trafford.
Alisema, “Pasi na shaka, nilikuwa na wasiwasi juu ya
hili, namna ya ajira yake ya umeneja wa Manchester United ilivyofanyika
halikuwa jambo la kupuuza na kuchukulia poa kabisa. Hiyo ndiyo ilipelekea
kufukuzwa kwangu.”
![]() |
| Boss wa sasa wa United akisalimiana na mtangulizi wake kwenye uwanja wa Anfield Jumamosi ya October 14. |
“Kwa upande wa misingi ya kazi siyo mbaya. ni mtu mwenye ushirikiano na yuko hivyo siku zote hata wakati alipokuwa msaidizi wangu.”
“Lakini mara nyingi huwa anashindwa kuimudu ghadhabu yake linapotokea la
kutokea.”
Van alikaribishwa
vizuri sana na watumishi wa klabu yake hiyo ya zamani pamoja na mashabiki na
akaendelea kusema “Nimepata kumbukumbu
nzuri sana na uhusiano wangu na watumishi pamoja na mashabiki ulikuwa safi tu
wakati nipo United.”
![]() |
| Mholanzi Louis van Gaal alifurushwa vilago vyake Manchester United siku mbili tu baada ya kunyakuwa FA Cup. |
Lakini mholanzi huyo
aliyenyimwa kazi zaidi ya 20 mwaka jana, ataendelea kuwakumbuka mashabiki wa
United ambao anaamini walikuwa ni kama kitu cha muujiza wanapofika uwanja wa
Anfield.
“Dakika kadhaa kabla ya filimbi ya mwisho kupulizwa, walikuwa wakiimba ’’’’’You’ll
Never Walk Alone’’’’’’’’’….hii inanipa msisimko kwenye mwili wangu wote. Oh’
inapendeza sana,” aliongeza Van Gaal.
Meneja huyo mstaafu wa
timu ya taifa ya Holland ameweka wazi kwamba alikuwa anapenda sana mchezo dhidi
ya Liverpool kitu kingine chochote wakati alipokuwa United.
“CEO wetu Ed Wood alikuwa ananiahidi chupa sita za Ribeiro Red Wine kila
tukiifunga Liverpool. Nikashinda mara nne, hivyo nikawa na chupa nyingi tu,” akaendelea
kusema kuwa “Huu ndiyo mchezo mkubwa
kabisa Wingereza.”
“Man City v Man United? Haiwezi hata kidogo kuisogelea ya Liverpool v
Man United. Hii ni kubwa kama ya Real Madrid v Barca, au ya Ajax v Fayenoord
nchini kwangu.”


No comments:
Post a Comment