Mwaka 2008 Frank Rijkaard alipigwa panga, Mourinho alikuwa kwenye mbio za kushika usukani, lakini badala yake akatimkia Inter.
Huenda Jose Mourinho
angetwaa ubosi wa Barcelona na kuiongoza timu hiyo ambayo wakati huo ilitawala
soccer la dunia huku ikiwa na kikosi kilichosheheni vipaji vya hali ya juu.
Meneja huyo wa sasa wa
Man United aliyeanzia kazi ya ukarimani na baadaye akawa kocha msaidizi wa Bobby Robison
na kisha akaungana na kikosi kazi cha Louis van Gaal kwenye ofisi za Nou Camp
maiaka ya 1990.
Lakini mpango wa kuwa
kocha mkuu wa klabu hiyo ungewezekana baada ya kupata mafanikio alipokuwa Porto
na Chelsea ambako alibeba ubingwa wa Champions League na Premier League.
Mwaka 2008 Frank
Rijkaard alipofukuzwa, Mourinho alikuwa kwenye mbiyo za kuiongoza Barca
iliyokuwa na kikosi chenye vichwa vinavyoheshimika duniani kote akiwemo Lionel
Mesi, Andreas Iniesta, Xavi Hernandez, Thierry Henry, Samuel Eto’o sambamba na academic ya timu.
![]() |
| Mourinho alifanya kazi na Bobby Robison na Louis van Gaal kwenye dimba hili la Nou Camp. |
![]() |
| Ni lini tutajua ukweli wa kilichotokea? |
![]() |
| Badala yake, Pep Guardiola akaichukuwa Barcelona. |
Lakini hakupata kazi na
badala yake akatimkia Inter Milan ambako alifurahia mafanikio ya ligi ya Italia
sambamba na yale ya Bara la Ulaya wakati huo Barcelona ikiendelea kung’ara
chini ya Guardiola.
“Haya mambo yanahusu kazi yangu ambayo binafsi naipa kipaumbele”
alisema wakati akifanya mahojiano na Telefoot.
“Labda nitakuja kulizungumzia hili siku moja nikiwa nimezeeka, tena
nimezeeka sana.”
“Kitu pekee nachoweza kusema ni kwamba mimi bado kocha mwenye matamanio
na malengo ya kuja kufanya vitu vipya.”
![]() |
| Mourinho akaenda zake Inter badala ya Barcelona. |
“Nina hakika kazi yangu haitaishia hapa Manchester United. Kuna siku
mwanangu anayeishi London, alienda Paris kutazama mchezo wa PSG na hakutaka
kutazama wa Manchester.”
“kwanini Paris? Kwasababu kuna vitu fulani maalum……..miujiza ya soccer,
ubora, vijana…..iko poa kiujumla.”




No comments:
Post a Comment