Binti
wa mfalme wa pop duniani, hayati Michael Jackson ameshindwa kuvumilia na
hatimaye kaamua kumchana yule mama maarufu kwa umbeya nchini Marekani baadaya
mambo ya familia kufanywa mada kwenye mtandao wa tweeter.
Alhamisi
ya jana Paris Jackson alijibu tweet ya bibi huyo wa miaka 53 iliyosema “mmelisikia
songombingo jipya la familia ya Jackson?”
![]() |
| Paris Jackson alipohudhuria kwenye tukio Beverly Hills huko California Marekani mwezi uliopita |
Tweet
ya bibi mpekuzi ilikuwa na picha ya mama yake Michael Jackson, bi Katherine
Jackson sambamba na ya mjukuu wake wa miaka 15 Prince Michael Jackson II (Blanket),
ikiongelea issue ya familia yake hususani upande wa malezi na ikawa linked
kweye Hot Topics Runtown.
![]() |
| Hii ni tweet ya Wendy William ikiuliza jambo la kizushi juu ya familia hii maarufu kabisa duniani |
Paris
naye baadaye kidogo akaongeza jibu lingine kwenye ile tweet huku post yake
ikiwa na picha yenye mchoro wa msichana anayeelezea jambo kwa hisia huku akiwa
ameinua mikono yake kana kwamba kuna kitu kinachoendelea lakini hakielewielewi
vyema. Ni kama anatamani atokee mtu mwenye kumnyamazisha huyu mama aache
kuiongelea hovyo familia ya hayati Michael Jackson.
![]() |
| Inaonekana Mungu amechoshwa na upuuzi wake akaamua kumwonjesha joto ya jiwe kidogo kwa kutoacha kuyasema majina ya watoto wa watu |
Kaka
mkubwa wa Paris, Prince Jackson mwenye miaka 20 alipata ajali ndogo ya pikipiki
jana asubuhi alipokuwa anaelekea chuoni kwake Loyola Marymount University
karibu na Playa Vista.
Prince
alishindwa kuimudu pikipiki yake wakati wa mvua hivyo akabebwa kwenye gari ya wagonjwa
na kukimbizwa hospitali ambako hakuonekana kuwa na majeraha makubwa, kulingana
na taarifa ya TMZ.
![]() |
| Wendy William, mama mtata mpekuzi, mbeya na mzungumza mambo ya watu |
Michael
Jackson ameacha watoto Paris na Prince aliozaa na Debbie Rowe ispokuwa huyu
Prince Michael II teknolojia ya upatikanaji wake bado haifahamiki.
Paris
anatarajia kuachia kazi yake ya filamu inayosimamiwa na mwongozaji kutoka
Australia, Nash Edgerton mwenye miaka 44, inafahamika kama Gringo na
itawahusisha David Oyelowo, Joel Edgerton, Amanda Seyfried na Charlize Theron
itaingia sokoni March 9, 2018.
![]() |
| Baba na wana: Paris na kaka yake Prince wanaonekana wakiwa na baba yao jijini London mwaka 2005 |






No comments:
Post a Comment