Atsu alihangaika sana kujiaminisha
apate namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Chelsea bila mafanikio, lakini sasa amekuwa
kivutio kikubwa Tyneside baada ya kusaini mkata wa uhamisho wenye thamani ya paundi
milioni sita.
Bado anakumbuka tukio
la wema aliotendewa wakati alipokuwa bado kinda na kuifanya ndoto yake kuwa
hai.
Alikulia kwenye kijiji
cha Ada Foah, kilicho mwendo wa saa moja
kutoka mwambao wa Accra, mji mkuu wa Ghana. Alikuwa mcheza mwenye uwezo mkubwa
wa kulitandaza soccer tangu utoto wake, akicheza kwenye viwanja visivyo na
nyasi huku vikiwa vimejaa mawe madogodogo kibao.
Siku moja kabla
mashindano ya majaribio yaliyoandaliwa na Fayenood’s West African Academy, mtu
mmoja asiyefahamika kabisa kutoka Achimota Accra alimpatia viatu vipya vya
soccer.
Alivivaa, akajisikia
vyema kabisa, akacheza vizuri sana na hatimaye akaanza rasmi harakati za kwenda
kucheza ligi kuu ya Wingereza akipitia timu ya Uholanzi na FC Porto ya Ureno.
“Walininunulia viatu bwana kwasababu walikuwa wanasema nina kipaji na
lazima nikifanyie kazi,” alisema Atsu alipokuwa anafanyiwa mahojiano kwenye
eneo la mazoezi uwanja wa Newcasctle. “Kwakweli
hii kitu sitaisahau kamwe.”
![]() |
| Christian Atsu, anatafuta namna ya kurudisha fadhira za wema aliotendewa |
“Kulikuwa na watu ambao walikuwa hawafahamiki na walikuwa wanataka
niendelee kufanya vizuri. Watu wa mji nilikokulia wakiona unakipaji kuna wakati
watakupatia pesa ya kukusaidia, au chakula ili kikujenge n ahata viatu pia.”
“Hivi ndivyo watu wa Afrika wanapenda soccer, watu usiowafahamu kabisa! Hivyo
ndivyo afrika ilivyo. Na hiyo ni roho ya kijumuia unayoweza kukutana nayo uwapo
Afrika.”
“Wanakuona, wanakufanya uwe na furaha na watataka kukusaidia.”
Mapema mwaka huu Atsu alianza
kumfikiria mtu aliyemtendea wema, ni baada ya Newcastle kumpandia dau la
kumnunua kutoaka Chelsea kwa paundi milioni sita.
Anaendelea kusema “Nilitaka sana kumwona mtu huyo, nikampanga
rafiki yangu amtafute, alikuwa anaitwa Joshua. Ni mtu mwema sana.”
“Alinunua viatu na sikuwahi kumwona tena. Sasa nimekuwa na ukaribu naye lakini
hataki chochote kutoka kwangu, lakini nilitaka japo nafasi hata kusema asante.
Kuna sababu
inayompeleka Atsu nyumbani kila wakati wa mapumziko. Mwaka huu alibeba mzigo wa
jezi na viatu vya Newcastle Unite pamoja na pipi na kuwapelekea watoto katika
kituo cha kulelea watoto yatima.
![]() |
| Mwezi June mwaka huu alitembelea na kutoa zawadi mbalimbali kwenye kituo cha kulea watoto yatima kijijini kwake |
Atsu alipmpoteza baba
yake mzazi akiwa na umri miaka 13 na mmoja wa ndugu zake 11 wa kuzaliwa.




No comments:
Post a Comment