Man U wanafikiria kumsainisha mtoto wa Phil Neville kutoka Valencia - SPORTSTAIN

SPORTSTAIN

Stay with us. Be informed

Friday, 6 October 2017

Man U wanafikiria kumsainisha mtoto wa Phil Neville kutoka Valencia

Ni dogo wa miaka 14 lakini sasa anatambulishwa kama David Beckham mpya na jina lake limeanza kutamkwa mara kwa mara kwenye viunga vya Manchester United.
Kwasasa Phil mtoto yupo miongoni wachezaji wa timu ya watoto ya Valencia inayojulikana kwa jina la Los Ches, na anafananishwa na Beckham kwasababu ya uwezo wake mkubwa wa kutumia guu la kulia kupiga mipira mirefu yenye macho.
Harvey Phil Neville aliingia Valencia mwaka 2015 baada ya baba yake kuteuliwa kuwa msaidizi wa kocha mkuu Gary Neville ambaye ni baba yake mkubwa. Lakini baba zake walifurushwa nje ya La Liga baada timu kufanya vibaya.

Harvey Neville yuko kazini
Hata hivyo Harvey alisalia nchini Spain baada ya kupatiwa mkataba mpya na sasa uwezo wake umeimarika na kuwa moja ya wachezaji chipukizi bora kabisa.
Kocha wa timu ya vijana ya Manchester United, Eric Harrison akiwa na wachezaji wake Ryan Giggs, Nicky Butt, David Beckham, Gary Neville, Phil Neville, Paul Scholes na Terry Cooke, 1992.
Na sasa chombo cha habari nchini Spain maarufu kama Super Deporte kinaripoti kwamba Man U wako katika mkakati wa kmrejesha nyumbani alikokulia baba yake.
Harvey Neville akionyesha namba ya fulana yake Valencia
Dogo anapata umaarufu nchini Spain
Inasemekana hata Tottenham Hotspurs wanamuwania Harvey Neville.
Harvey alianza maisha ya soccer kwenye timu ya watoto ya Carrington baadaye akaenda Manchester City kabla familia yake kuhamia Spain.
Harvey ataweza kupita vyema nyayo za baba zake?
Baba yake “Phil Neville” anajivunia sana maendeleo ya mwanae kiasi amekuwa na utaratibu wa kurekodi na kurusha mara kwa mara video za mwanae akiwa na timu yake ya Valencia kiasi cha kukamata hata macho ya David Beckham kwenye kurasa yake ya Instagram.
Phil Neville na familia yake



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad