Mkongwe wa muziki
nchini Marekani, Lionel Richie anatamani amzuie
bintiye wa miaka 19 kutoka kimapenzi na mkali wa bata za kimataifa Scott
Disick.
Lionel Richie
ameshindwa kuzuia hisia za anachofikiria juu mahusiano hayo ya bintiye na bwana
Scott.
Sofia ana miaka 19 na
huyo baba wa watoto watatu mwenye miaka 34, juzi kati walionekana hadharani wakiwa
kwenye mtoko wa nguvu na kuuthibitishia ulimwengu kuwa wanatoka kimapenzi na
wameshibana sana tu.
Lakini mzee wa “All
Night Long” ameweka wazi kuwa yeye anawasiwasi sana na mahusiano hayo.
“Nimekuwa na hofu?.........mimi ni baba,……….wacha kabisa bwana,” aliongea
hivyo alipozungumza na US Weekly.
![]() |
| Richie na Sofia |
![]() |
| Rich na Sofia miaka ya hivi karibuni |
Alipoulizwa kama yuko
poa kuyakubali mahusuano hayo, akasema: “ninaogopa
kiasi nahisi kufa……….unanizingua au siyo?”
Sofia na Scott
walifotolewa mapicha wiki hii wakiwa wamejituliza PDA nchini Mexico kama njia
ya kufurahia penzi lao jipya.
Baba wa watoto watatu na binti mwanamitindo waliyaanika mapenzi yao
hadharani kwa video waliyojirekodi wakikisi wiki kadhaa zilizopita na baadaye
wakaonekana wakitumbukia kwenye maji na kuogelea huku wakiwa na furaha iliyopiliza.
Chanzo cha habari cha
awali kiliwaambia watu kuwa Sofia Richie amemkubali sana Scott.
![]() |
| Scott Disick na Sofia Richie |
Wambeya nao hawako nyuma,
wanasema kuwa Scott na Sofia hawakai mbali, muda wote wanakuwa
pamoja.
“Scott anampetipeti sana Sofia, anamfungulia mlango wa gari na analipia
kila kitu kwa Sofia” walidai wananzengo.
![]() |
| Sofia Richie |
![]() |
| Scott Disick |
Scott ameshawahi kuwa
kwenye mahusiano na wanawake kadhaa tangu alipoachana na aliyekuwa kuwa mke
wake mwenye watoto wake watatu Kourtney Kardashian, mwaka 2015.
Kuna wakati alihusishwa kuwa mahusiano na mcheza sinema Bella Thorne, ambaye inasemekana kuwa ana umri
kama wa Sofia.
Habari hii
imetafasiriwa na Davis Mwakalosi kwa hisani ya mtandao Mirror. Tafadhari wasiliana
nasi kwa njia ya email sportstz17@gmail.com
au tembelea, ku-like na ku-follow account zetu za Facebook (sportstain), Instagram (sportain_tz) na Tweeter
(sportain_tz).







No comments:
Post a Comment