Kama ingekuwa ni
kibongobongo basi tungesema pale jijini London kwenye uwanja wa Highburry kuna
misumali mikali sana, kwa maana mpaka sasa Arsenal wana majeruhi sita kutoka
kikosi cha kwanza.
Ndiyo kwanza tuna miezi
mitatu tu ya msimu huu wa ligi ya EPL lakini tatizo la majeraha kwa Arsenal
linaonekana kushamiri siku hadi siku.
Wenger sasa atalazimika
kupamabana na hali yake bila ya wachezaji wake kadhaa wa kikosi cha kwanza huku
akiendelea kufanya dua zake zote michezo ya kimataifa ya wiki hii isimwongezee
matatizo zaidi.
Watu wa football.london report kamili
kutoka chumba cha matabibu wa The Gunners.
Mesut
Ozil
![]() |
| Ozil atakuwa nje ya dimba kwasababu ya tatizo la goti |
Aina
ya jeraha : uvimbe
kwenye goti.
Nje
ya uwanja : alicheza
dakika za mwisho za mchezo walioshinda dhidi ya West Brom September 25.
Anatarajiwa
kurejea : kwenye
mchezo dhidi ya Watford October 14.
Maoni
ya Wenger : baadhi
ya wachezaji hawaenda kwenye michezo ya kimataifa. Mesut Ozil anatatizo la
goti.
Laurent
Koscielny
![]() |
Aina
ya jereha : mfupa
wa kisigino
Nje
ya uwanja :
mchezo walioshinda dhidi ya West Brom September 25.
Anatarajiwa
kurejea : kwenye
mchezo dhidi ya Watford October 14.
Maoni
ya Wenger : baadhi
ya wachezaji hawataenda kwenye michezo ya kimataifa. Mesut Ozil anatatizo la
goti.
Danny
Welbeck
![]() |
| Welbeck anajeraha kwenye nyonga |
Aina
ya jereha : kinena
Nje
ya uwanja :
mchezo waliotoka sare 0-0 dhidi ya Chelsea September 17.
Anatarajiwa
kurejea : kwenye
mchezo dhidi ya Watford October 14, au ikizidi sana basi itakuwa na Everton
October 22.
Maoni
ya Wenger : bado
hatufahamu jeraha lake kinena litamsumbua kwa muda mrefu kiasi gani ni hakika
kwamba atakosa michezo ya kimataifa ya wiki hii, lakini imani yetu kuwa sawa
kwenye mchezo dhidi ya Watford.
Francis
Coquelin
![]() |
| Coquelin anatarajiwa kurejea dimbani hivi karibuni |
Aina
ya jeraha : tatizo la msuli
Nje
ya uwanja :
mchezo walioshinda 3-0 dhidi ya Bournemouth September 9.
Anatarajiwa
kurejea : kwenye
mchezo dhidi ya Everton October 22.
Maoni
ya Wenger : Coquelin
hataweza kushirki michezo hii ya kimataifa pia anatatizo la msuli.
Santi
Cazorla
![]() |
| Mnanikumbuka? |
Aina
ya jeraha : mfupa wa kisigino
Nje
ya uwanja :
tangu October 2016.
Anatarajiwa
kurejea : January
2018.
Maoni
ya Wenger : dalili
za awali zinaonyesha maendeleo mazuri, lakini bado hajaweza kucheza kwa muda wa
mwaka mmoja na nusu.
Hayuko kwenye mazoezi
kamili ya timu, anahitaji michezo michache akiwa na timu ya akiba. Laikini
nafikiri kila kitu kiko sawa na atarejea kutoa huduma baada ya Christmas.
Calum
Chambers
Aina
ya jeraha : nyonga
Nje
ya uwanja :
mchezo walioshinda dhidi ya Doncaster September 20.
Anatarajiwa
kurejea : kwenye
mchezo dhidi ya Everton October 22.
Maoni
ya Wenger : Chambers
ameumia tena tena nyonga yake, jerha linaonekana siyo kubwa sana………lakini
nadhani anahitahi muda wa wiki moja au mbili aweze kurudi kwenye hali ya
kawaida






No comments:
Post a Comment